GET /api/v0.1/hansard/entries/1441156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1441156,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441156/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ODM",
"speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
"speaker": null,
"content": "Pia, kuna kipengele ambacho kinahusu maneno ya kuongeza bei kwa vifaa vya kufanya utafiti wa ugonjwa wa saratani. Kwa hivyo, mimi kama Mjumbe wa Butere ninapinga Mswada huu wa Fedha, 2024. Wenzangu ambao wako kwa Serikali watimize ile ahadi ambayo waliambia Wakenya. Tunataka kuona mama mboga akifaidika katika Serikali, boda boda na mtu wa chini ambaye ni hustler akifaidika. Tunataka kuona viwanda vikinawiri wala sio kuweka ushuru wa juu. Mimi kama Mjumbe wa Butere ninataka niende katika rekodi kwamba nimepinga Mswada huu na ninajua Wakenya wengi wako na sisi tukipiga kura kuupinga Mswada wa Fedha mwaka wa 2024."
}