GET /api/v0.1/hansard/entries/1441190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441190,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441190/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Voi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Khamis Chome",
    "speaker": null,
    "content": "Ninakubaliana nao. Sababu za msingi ni kuwa Mswada ulivyotengenezwa tangu awali, sio mzuri kwa uchumi, wananchi, waekezaji na nchi kwa jumla. Nimeona nia na lengo la kuwahadaa wananchi. Hii ni kwa sababu yale yaliyokuwa yakiuma sana tumeambiwa yataondolewa. Lakini, swali ni, kwa nini mambo hayo yalikuwa kwa Mswada huu mwanzoni? Vijana wetu wameongea na kujitokeza. Inahuzunisha na kufedhehesha kuona kuwa maafisa wa polisi wamewafuata kuwagadhibu na kuwasumbua, ilhali, wanaenda kulingana na Katiba hasa Article 37, ambayo inawaruhusu kukutana, kuandamana na kupeana petition . Ingekuwa vizuri kwa nchi yetu kama tungedumisha demokrasia na kwenda kistaarabu. Mhe. Spika, utunzi wa sheria unatakikana kuzingatia hali ya wananchi. Hata ukiiangalia vizuri, kwa jina la Kiingereza, Mswada huu unanuia kurekebisha Mswada mwingine. La msingi ni kuwa tufanye iwe rahisi. Malengo ya kukusanya ushuru hayakuafikiwa. Sababu kubwa hasa ni kuwa hali ya uchumi imekuwa ngumu. Wawekezaji wameondoka na kazi zimepotea. Mswada huu ungelenga kupunguza yale yaliyokuwa yakiwakaza wananchi ama ubakie vile vile."
}