GET /api/v0.1/hansard/entries/1441193/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441193,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441193/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "Kwanza Mhe. Spika, ninaunga mkono Mswada ambao umeletwa kwenye Bunge hili ili tuujadili kama Wajumbe. Tunaelewa tulikuwa na Waziri wa Hazina ya Fedha na Mipango ya Kitaifa wiki mbili zilizopita. Mwenyewe alipeana taarifa ya mahitaji ya kila Wizara. Aligusia sana Wizara ya Elimu na Ile ya Kilimo na Mifugo. Sisi sote tunaelewa kwamba ni muhimu sana kusaidia wakulima ambao ndio wengi miongoni mwetu. Ninaelewa kwamba katika kilimo tumeangalia kila sekta ndogo wakiwemo wakulima wa matunda yaani horticulture na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa. Nimefurahi sana kwa kuwa kuna pesa imetengwa ili wakulima wa maziwa wajengewe viwanda vya kuhifadhi na kuboresha maziwa yao. Hii ndio itapatia nafasi vijana waajiriwe kazi. Pia, itapeana usaidizi mkubwa sana kwa wakulima wetu."
}