GET /api/v0.1/hansard/entries/1441195/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441195,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441195/?format=api",
    "text_counter": 271,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "Mswada huu ni wa maana kwa vile hakuna sababu ya Serikali yetu kuendelea kuomba pesa kutoka nchi nyingine. Pesa tunazokopa kwa riba ya juu zitalipwa na watoto na wajukuu wetu. Ni vyema sisi sote kama viongozi wa nchi hii tuwe na nia nzuri. Wengi tunaongea mambo ya barabara, maji na stima. Haya yote ni maendeleo. Kwa hivyo, ninachukua nafasi hii kusema, tulichaguliwa katika Bunge hili ili tuongee juu ya majukumu yetu kama viongozi. Jukumu kuu ni kuwaambia Wakenya ukweli kuhusu yanayoendelea. Hakuna haja tunyamaze kama viongozi na baadaye tukope pesa kutoka nchi nyingine ndiyo tutatue shida zetu."
}