GET /api/v0.1/hansard/entries/1441210/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441210,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441210/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": "Wananchi kule nje wanaandamana kwa sababu ya kutozwa kodi katika Bajeti ambayo ilikuwa imeletwa hapa. Yale makadirio ya kutoza kodi ndiyo yamefanya watu waandamane. Ninaunga mkono wale wanaoandamana kule Kilifi leo. Waliona katika orodha ya kutozwa ushuru kuna mkate na magari ya mwananchi wa kawaida. Watu kama Mhe. Ichung’wah na Mhe. Osoro ni vijana wadogo ambao wamefura vichwa. Hawatumii magari siku hizi. Wanatumia ndege ili waende kwa kila mkutano. Ndiyo maana wanasema magari yatozwe ushuru. Wanataka kutoza ushuru vyombo vya kupima saratani."
}