GET /api/v0.1/hansard/entries/1441231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441231/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Watu wa Lamu Mashariki tumekuwa tukitoa ushuru kama Wakenya wengine. Maeneo bunge mengine yameendelea. Nahisi tuzidi kutoa ushuru sana ndiyo nasi watu wa Lamu Mashariki tupate maendeleo. Ninaunga mkono kwa dhati nikiwa na imani kuwa Serikali hii ndiyo itatuunganisha sisi na Wakenya wengine. Lazima tuwe wavumilivu na tufikirie Wakenya wengine. Wengine wetu bado tuna hamu na maendeleo ambayo hatujapata. Nyinyi mlio mjini mna barabara na stima kila pahali. Mmeshiba. Kule kwetu sisi husema walioshiba samli wanatoa miba. Kwetu bado tuna njaa ya maendeleo. Hatuwezi kupinga pesa kupatikana. Toeni ushuru, wacheni mchezo. Kuna watu wanaumia. Ushuru ndiyo kuendelea kwa nchi. Sisi tunavumilia."
}