GET /api/v0.1/hansard/entries/1441497/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441497,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441497/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwanza, nawapatia Wakenya kongole kwa kusimama kidete na kuweka kilio cha haki katika Mswada huu wa Fedha. Tunazungumzia Ripoti na Mswada wenyewe. Ripoti inasema wataweka Kifungu 66 waweze kuongeza pesa kwa mafuta kutoka Ksh18 mpaka Ksh25. Tunasisitiza hapa kuwa jambo hilo halitafanyika. Jambo hilo lisiwekwe kwa Kamati ya Jumba nzima sababu iwapo itaongezwa, basi itakua yale yote ambayo yamerekibishwa ni bure. Kwa sababu ukiongeza bei ya mafuta, utakuwa umeongeza gharama ya uchukuzi, gharama ya kutengeza bidhaa, na bei ya kila kitu itapanda. Jambo la pili, iwapo tunataka kukimu bajeti yetu, haiwezi kuwa njia ni moja tu ya kuweka ushuru kwa Wakenya ambao ni walalahoi na wamefika ukutani. Lazima tubadilishe mbinu, tuwe na mbinu mbadala ya kufufua na kujenga viwanda na kutafuta njia ya kupata mapato kwa taifa letu kupitia rasilimali nyingi tulionazo. Haya mambo ya kuongeza kodi ya mazingira… Tumezungumzia kwamba sodo na nepi kuwa zinapatikana kwa wingi hapa Kenya. Lakini kwa hivi sasa, akina Mama ambao wanawakilisha kaunti wanasubiri sodo na wanaambiwa ziko China wazingoje zije. Hiyo ni kumaanisha hatuna uwezo thabiti wa kuwa na sodo na, hivyo basi, afya ya akina mama haswa katika mambo ya health itakuwa na matatizo iwapo tutaongeza jambo kama hili. Jambo la tatu ni mambo ya mafuta ya kutoka kwenye miti na Wanyama, ile kwa Kiingereza inaitwa edible oil . Kwa nini isipunguzwe na kutolewa kabisa iwekwe sufuri ushuru? Hii ni bidhaa ambayo inatumika na Wakenya wengi walalahoi. Kwa hivyo, hili jambo lazima tulitoe. Jambo jingine ni hili: Nasikitika sana na sijui ni nani amepeana mawaidha ya kuweka ushuru kwa mkate na mifuko ya majani. Jamani, yule aliyetoa mawaidha hayo ninamwambia shetani ashindwe kwa sababu sisi Wakenya mkate tunaupenda, twautumia sana kwa chai, na ndio kiamsha kinywa chetu. Katika huu Mswada, kuna mambo mengine ambayo yamejificha na yanatuathiri sana. Kwa mfano, stove za kupika hutumika sana na Wakenya wengi ambao hawawezi kununua meko za gesi. Hizo pia zimeongezewa ushuru. Tunapigana na janga la malaria, lakini leo tunaambiwa mosquito repellent ama ile dawa ya kujipaka ili kusudi watu wasiumwe na mbu na kuleta malaria pia imeongezwa ushuru."
}