GET /api/v0.1/hansard/entries/1441506/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441506,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441506/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Mheshimiwa Spika, bidhaa zile ambazo zinatoka nje ambazo tunasema tutazitoza ushuru lazima tuwe waangalifu tusije tukaweka ushuru katika bidhaa ambazo sisi kama taifa bado hatujatengeneza viwanda vya kutosha vya kutengeza hizo bidhaa kama vile clinkers . Sasa hivi, tunajenga majumba ya bei nafuu na tunatumia material nyingi sana na hivi basi hatuna viwanda vya kutosha vya kutengeza bidhaa kama hizo. Kwa hivyo, lazima tuangalie wakati mwafaka wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za kutoka nje wakati tumetimiza na kuwa na uwezo kama taifa la Kenya. Vile vile, tuliambiwa kwamba magari ni mapato na kwamba tutoe ushuru. Nasema magari si mapato. Magari ni ile tunasema asset au rasilimali kwa Kiswahili na huwezi mtoza mtu ushuru katika rasilimali. Jamani tupunguze matumizi ya kiholela katika ofisi zetu, Ofisi ya Naibu wa Rais inahisi kurekebishwa na mabilioni za pesa. Ukiangalia bei ya kununua hio ofisi na bei ya marekebisho ni tofauti sana. Lazima tuangalie ufujaji wa pesa tuweze kusaidia taifa la Kenya, lakini tusitegemee mambo ya ushuru pekee tukaona tunaweza kukimu bajeti yetu. Sisi kama Wakenya tuendelee kusimama kidete, tusingoje wanasiasa tunapoona mambo yanatukwaza hasa haya ya uchumi. Tusimame kidete tusikie sauti zetu zikizungumziwa. Jambo jingine ni kwamba…"
}