GET /api/v0.1/hansard/entries/1441660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441660,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441660/?format=api",
    "text_counter": 406,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Sana, Mhe. Spika. Mwanzo nachukua fursa hii kuwashukuru Wakenya. Wenzangu wengi wamesimama hapa na kusema tuwashukuru Wabunge wa Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa. Lakini mimi nimesimama kuwashukuru Wakenya. Kwa mara ya kwanza, tumeweza kuona nguvu na umoja wao. Tunapoungana na kusema no au kukataa jambo, halitapita. Jambo la kwanza ni ushirika wa umma. Nasimama hapa kuupinga vikali Mswada huu wa fedha ambao umewasilishwa mbele yetu. Watu wangu wa Malindi wanapinga vikali maswala ya kuongezwa ushuru kwa mkate, pampers na sanitary pads. Tayari vile hali ya maisha ilivyo ngumu, wanasema hawataki tena kuona ushuru wa aina yoyote ukiongezewa. Sisi Waswahili tuna msemo kwamba: ‘Unapopatiwa chakula, usije kusahau mpaka ukala ile sahani’. Tulipokuwa tukijadili Mswada wa Fedha wa 2023, kulikuwa na mambo mengi ambayo tulikuwa tumekataa lakini hayo mambo yakapita. Ninavyoona, huu Mswada ulikuwa unataka kupitisha mambo mengi zaidi lakini safari hii, Wakenya walikuwa chonjo. Waliweka miguu yao chini na kukataa udhalimu ambao ungetendeka. Nawaomba wananchi kwamba kunapoitishwa vikao vya kutoa maoni kuhusu miswada – kwa kimombo, public participation – wajitokeze kwa wingi ili mapendekezo yao yasikizwe na kujumuishwa kwenye sheria zitakazoidhinishwa na Bunge la Taifa. Kabla ya kuzungumza kuhusu huu Mswada tunaoujadili sasa, inafaa tuangalie Mswada wa Fedha wa 2023 uliweza kutusaidia kivipi sisi kama Wakenya. Tunafaa tujiulize iwapo gharama ya maisha ilibadilika, mazingira ya kazi yalikuwa mazuri kwa watu wetu na Mswada huo umeweza kutufikisha wapi. Tumetimiza malengo yetu na hio bajeti? Kuna vitu ambavyo tulipitisha kupitia Mswada huo, yakiwemo maswala ya Hustler Fund na Housing Levy. Tunapaswa kujua iwapoa tulitimiza malengo hayo. Nikimalizia, Wakenya hawana shida na kulipa ushuru ninavyowaelewa. Uchungu wao sasa hivi tunapozungumza kuhusu bajeti ya trilioni tatu ni matumizi ya fedha hizo. Hiyo ndio maana tuliwaona vijana wetu wadogo wakienda barabarani kuandamana. Tatizo ambalo tuko nalo sasa hivi ni ufisadi. Tunapozungumiza kuhusu ufisadi, fedha zote za bajeti hutoka kwa Wakenya. Tunaona ufisadi unavyoendelea. Mawaziri walio na kesi za ufisadi huwachiliwa. Mambo kama hayo ndiyo yanayozidi kuwatia Wakenya machungu. Walioshikana upande wa Serikali wakienda kwenye mikutano ya harambee, mtu aliye na mshahara sawa na wangu anachanga karibu Ksh30 milioni ilihali kuna vijana ambao hawana kazi wala shilingi. Kwa hivyo, tunataka marekebisho kuhusu jinsi pesa za umma zinavyotumiwa, na ufisadi umalizike hapa nchini Kenya. Naupinga vikali Mswada wa Fedha, 2024."
}