GET /api/v0.1/hansard/entries/1441689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1441689,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441689/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "Kwanza, nawapongeza Wakenya wote waliojitokeza jana kuandamana ili kutoa hisia zao kuhusu Mswada huu wa Fedha wa 2024. Pia, nawapongeza wote walioshikwa wakitetea haki yao. Hao ni mashujaa tulionao wa karne hii. Napinga Ripoti na huu Mswada wa Fedha wa 2024 kwa sababu kadhaa. Hatuwezi inua uchumi wa nchi kwa kutoza ushuru peke yake. Tunafaa kujiuliza mazingira tuliyoweka kusaidia mwananchi apate pato ndiposa aweze kutoa ushuru. Jibu ni kuwa hatujaweka njia mwafaka ya kusaidia watu wafanye biashara. Mapendekezo ambayo yamefanywa na Kamati ya Kiidara ya Fedha na Mipango ya Taifa kuondoa ushuru wa mkate walivyokuwa wamependekeza ni kwa sababu Wakenya walisimama na kusema hawataki hayo. Ndipo wamekuja kusema kuwa wameleta mapendekezo. Wamepanga haya mapendekezo lakini hayako katika Mswada wa Fedha wa 2024. Haya mapendekezo yanawezapita ama yasipite. Yasipopita, tutafanya vipi na tayari mmependekeza ushuru uongezeke? Tumesema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}