GET /api/v0.1/hansard/entries/1441691/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441691,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441691/?format=api",
    "text_counter": 437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": "Serikali hii ilikuwa inasema kuwa inatambua mtu wa boda boda na mama mboga. Huyu mama mboga yuko wapi kwa hii Bajeti? Huku unasema umeondoa kuongezwa kwa ushuru wa mkate na ushuru wa tahiri, lakini hapo hapo umemuongezea bei ya mafuta. Ukipandisha bei ya mafuta, gharama ya bidhaa zote muhimu itapanda; ukiongeza bei ya mafuta, boda boda na mama mboga ambao mliwatumia wakati wa kampeini zenu mmewaweka wapi?"
}