GET /api/v0.1/hansard/entries/1441695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1441695,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441695/?format=api",
"text_counter": 441,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii niweze kupeana maoni yangu kuhusu huu Mswada wa Fedha 2024/2025. Mimi pia ni kati ya wale Wabunge ambao wametumiwa jumbe nyingi sana na wakaazi wa Ganze wakiniambia niupinge Mswada huu kwa sababu hauwafai. Wengi wa wale ambao wamekua wakinitumia jumbe nimekua nikiwauliza ni vipengele gani katika Mswada huu ambavyo wanaona viko na shida. Ni wachache ambao waliweza kunitumia jumbe wakiniambia kuna vipengele fulani fulani ambavyo wanaona vina shida na wangetaka viondolewe ama virekebishwe ama Mswada huo uweze kukataliwa kabisa."
}