GET /api/v0.1/hansard/entries/1442102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442102,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442102/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "iliratibia mkate, edible oils na vitu vinavyomgusa mwananchi wa kawaida kama vile magari, ilikuwa njia moja ya kuwaondolea Wakenya shetani iliyobaki ndani mwa hii Bill . Wakenya wamemakinika na ukiwaona wanaingia barabarani wenyewe bila ‘Baba’ jua kuna shida. Hii Finance Bill, 2023, Wakenya wameikataa maana nao, walilazimishiwa Housing Levy. Tusidanganywe kuna kitu Wakenya wamekubaliana nayo. Mwenye alipanga mambo ya kutoza ushuru mingi kwa mkate alifikiria kitu gani? Ninapoangalia pesa ambazo zimekadiriwa kukusanywa na matumizi yake, Wakenya wamefinywa. Hata ukipiga paka na kumfungia ndani mwa chumba, atakung’ata. Wakenya sasa wameanza kutuandama pamoja na Rais na messages maana wameamka. Tutacheka leo, wengine wakiskia raha na wengine watapiga kura ‘Y es’ lakini mkumbuke huu Mswada sio wenu tu. Utadhuru vizazi zijavyo na utafika wakati ambampo hautakuwa Bungeni na wazazi, watoto na ndugu zako hawatakuwa na uwezo na wataskia kugandamizwa. Kwa hivyo, tunapotunga sheria, tuangalie kama ni ya kusaidia ama kumharibu Mkenya wa kawaida. Bajeti ambayo imetengewa Ofisi ya Rais ni karibu Ksh7.9 billion, ilhali ya Naibu wake imeratibiwa Ksh4.5 billion . Hawajaonyesha ratiba ya vile hii pesa itatumika pale. Pesa ambazo zinaenda kwa mwananchi ni duni kabisa. Ukiangalia upande wa Health, wanaingiza na mkono huu kisha kutoa 16 per cent kwa wagonjwa wanaougua saratani . Tunataka kupigana na saratani. Akina mama wanaugua saratani. Huu ugonjwa umewafikia maskini ambao hawajiwezi. Wakenya na Wabunge wenzangu, tunaelekeza wapi taifa hili ikiwa tunaongeza"
}