GET /api/v0.1/hansard/entries/1442105/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442105,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442105/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Mkate, maziwa na kadhalika pale ndani ya State House ni Ksh13 bilioni. Naiangalia na kusema jamani tuoneni haya. Mgala muuweni ila haki yake mpeni. Huyo tunayemnyang’anya hizi pesa kwenda kufund vitu vya starehe ni mtu anayelia kwa Mungu kila siku asubuhi akiamka: “Mwenyezi Mungu, ninatoka ndani ya nyumba yangu. Nishukishie riziki kwa mikono yangu niweze kulea watoto wangu.” Lakini, tunaenda kukata katika ile ruzuku yake. Kwa mfano, mkenya anatoka nyumbani na mshahara wake ni Ksh50,000. Katika Ksh50,000, Ksh24,000 yote inakatwa na Serikali. Hiyo ni tax peke yake. Mara ni Pay As You Earn (PAYE) sijui na nini. Kisha anabaki na Ksh26,000 huku ana gharama ya stima na maji atakayolipia. Anafaa anunue unga na apeleke mtoto shule. Wakenya wamechoka. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}