GET /api/v0.1/hansard/entries/1442196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442196,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442196/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ". Amezungumzia ugavi wa bajeti ambao unakuja kwenye mkoba wa hazina ya Mama Kaunti na mkoba wa hazina ya NG-CDF. Mhe. Spika ukipiga hesabu, ugavi huo wa Ksh500 milioni unaenda kwa wananchi sio kwa viti vya akina mama. Unaenda kwa wananchi katika kazi ya empowerment ili wakuze uchumi. Pia, unaenda katika ukuzaji uchumi. Lakini, zile pesa ambazo tunaulizia ni zile ambazo zimeenda kwa makadirio ambayo hayachangii kukua kwa uchumi, bali ni ya mambo ya starehe. Kwa hivyo Mhe. Osoro, usiwadanganye wananchi kwa kusema kwamba wameletewa Ksh500 milioni wakati mkono wa pili umechukua mabilioni ya pesa. Ahsante sana."
}