GET /api/v0.1/hansard/entries/144237/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 144237,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144237/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Musila",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Defence",
    "speaker": {
        "id": 94,
        "legal_name": "David Musila",
        "slug": "david-musila"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, naomba kujibu. (a) Ni kweli kwamba uchunguzi wetu wa awali ulithibitisha kwamba tukio hilo lilitokea kule katika eneo la Nairoborkeu, tarafa ya Loroki, wilaya ya Samburu ya Kati mnamo Jumamosi tarehe 13 Juni, mwaka huu. Nasikitika kwamba kutokana na kisa hicho, mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 12 kwa jina Tetema Lekariekeu aliuawa na mlipuko wa bomu baada ya yeye kulichukua bomu hilo na kulipigisha kwa mwamba wa mawe. (b) Wanajeshi wa Kenya watafanya kazi ya kutafuta na kutegua mabomu na vifaa vingine ambavyo viko katika maeneo hayo ili kuyafanya salama kwa jamii hiyo. Ahsante, Bw. Naibu Spika."
}