GET /api/v0.1/hansard/entries/1442397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442397,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442397/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, nasimama kuunga mkono Hoja hii ya kuahirisha vikao vya Bunge letu la Seneti kwa moyo mzito sana. Tunasimama hivi leo hapa tukiwa tumewapoteza ndugu zetu na watoto wetu. Hapa sio pahali pengine katika Kenya ama mbali na maeneo ya Bunge, lakini tumeweza kupoteza watoto wetu ndani ya maeneo ya Bunge ambapo walipigwa risasi. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha sana. Nikisimama hapa, ninajua kuna akina mama wengi sana katika Kenya hivi leo ama ndugu zetu wa kike na kiume na Wakenya kwa jumla, wamepoteza ndugu zao na jamii zao kote katika Kenya. Hata hivyo hatujajua hesabu ya wale waliopoteza maisha. Kwa hivyo, katika shinikizo hili, nakubaliana na maahirisho ya vikao vya Seneti. Tunataka tuwape nafasi wale ambao watakuwa wachunguzi kuweza kujua ni nini kilitendeka, akina nani waliingia hapa na akina nani waliongoza hususan kile kikosi cha polisi kilicho ingia hapa ndani ya maeneo ya Bunge, wakikimbiza ama wakiwafuata waliokuwa wakiandamana. Pia, tunataka kujua ni kina nani wale waliwapiga risasi waandamanaji wakiwa ndani ya maeneo ya Bunge na kumuangusha Mkenya mwingine kwa risasi ili yeye aweze kuonekana ni jemedari. Bw. Spika, tunajua maeneo ya Bunge ni maeneo ambayo hayatakikani watu ambao hawatakikani kuingia ndani ya hili Bunge. Bunge ni eneo ambalo limechungwa sana lakini si ya kwamba wewe unaweza kufyatua risasi na kuua Mkenya. Kwa hivyo, tunakubaliana kwamba tuahirishe vikao vya Seneti ili uchunguzi ufanywe ili tuweze kujua ni askari yupi alichukua ile bunduki yake kisha akaweza kumwangalia Mkenya na kumfyatulia risasi. Kama tunaahirisha vikao ni kwa sababu ambazo zina mwafaka. Jambo lingine ambalo tunataka kujua ni kwamba ilikuwaje hawa askari ambao walikuwa pale mbele ya majengo ya Bunge kuweza kukubaliana ama kuwachilia watu kuingia Bungeni ama ilikuwa ni makusudi kuwatega wale waliokuwa wanafanya maandamano kwa kufungua malango kisha wakawaacha kuingia ndani? Tunataka kujua haya kwa sababu askari waliokuwa pale nje walikuwa na jukumu la kuwakinga wale watu waliokuwa wakifanya maandamano au wale wanaojulikana kama Generation Z. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}