GET /api/v0.1/hansard/entries/1442398/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442398,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442398/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tunaelewa ya kwamba sisi kama Wabunge tuko hapa na haya ni maeneo ambayo yanaingia watu wa nje kwa ruhusa ya inayotolewa hapa. Tuliona maroli ya polisi ambayo yalikuwa yakiwazuia watu ili wasiweze kuingia. Ilikuwaje waliruhusiwa na mlango ukafunguliwa na wakaingia ndani? Hilo ni jambo moja ambalo tunaweza kusema ya kwamba tunataka uchunguzi ufanywe ndio sababu tunatoa nafasi hii. Yale yanayosemwa ya kwamba Bunge liliweza kuingiliwa na likaharibiwa na maeneo mengine kama maeneo ya kula chakula na maeneo ambayo walikuja wakaangusha hizi bendera zetu. Hata hivyo hao walikuwa Wakenya lakini tunasema ya kwamba, katika maeneo hayo ambayo tumesema, kama ni mambo ya chakula, sisi hatuji hapa kwa sababu ya kula chakula. Tunakuja hapa ili kujadiliana na kuangalia ni mbinu gani tunaweza kusaidia Wakenya. Bw. Spika, ninasema ya kwamba, wale walioweza kuingia na pengine wakaenda maeneo mengine wakaharibu wanajulikana. Kwa hivyo, tunataka uchunguzi ufanywe ili tuweze kujua ni akina nani wale waliingia katika maeneo haya na kuweza kuharibu ama kufanya vitendo ambavyo havifai. Sisi tunasema ni sawa tunaweza kuahirisha vikao na tuwape nafasi ili waweze kufanya uchunguzi wao. Kwa hayo mengi ---"
}