GET /api/v0.1/hansard/entries/144242/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 144242,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144242/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Musila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 94,
        "legal_name": "David Musila",
        "slug": "david-musila"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, kama vile nilivyosema hapo awali, ni kweli kuwa kisa hicho cha kusikitisha kilitokea na ningependa kulijulisha Bunge kwamba Jeshi la Kenya lilikuwa likifanya mazoezi katika sehemu hiyo katika miaka ya 1980s na 1990s. Hivi sasa, tumeacha kutumia sehemu hiyo kwa mazoezi. Bw. Naibu Spika, vile ningependa kusema, haswa kwa Mheshimiwa aliyeuliza Swali hili na wengine ambao wanaishi katika sehemu ambazo mazoezi ya jeshi yanafanyika, tunafanya juhudi kubwa kila wakati baada ya mazoezi kutafuta vifaa vyovyote, vikiwemo mabomu, risasi na vyombo vingine; tunaviokota na kuvipeleka kwengine! Lakini, haiwezi kukosa kwamba moja ya mabomu yanaweza kukosa kuonekana. Kwa hivyo, vile ningependa kuuliza kupitia kwa Wabunge na maofisa wetu wa kushughulikia utawala na usalama ni kwamba wawajulishe wananchi kwamba wakipata vifaa vyovyote katika sehemu hizo, wapige ripoti. Kama vile kisa hicho cha kusikitisha kilipotokea, kijana huyo alichukua kifaa hicho - pengine hakujua ni nini - na akakipigisha kwa mwamba wa mawe ndipo kikalipuka."
}