GET /api/v0.1/hansard/entries/1442430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442430,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442430/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu. Pia, ninachukua nafasi hii kutuma pole zangu kwa wale vijana waliuwawa, walioumizwa pia na wale wako hospitalini kwa ajili ya maandamano. Jana, mimi, Seneta wa Pokot na Wajumbe sita kutoka Bunge la Taifa tuliingia kwa ambulensi ili tuweze kutoka kwa majengo ya Bunge. Tulikutana na vijana waliokuwa wanasimamisha ambulensi na sisi tulikuwa kwa moja. Hiyo gari imenyoroshwa na mawe, mbele, nyuma, katikati na kila mahali. Bw. Spika, leo ungesikia vifo vya Wabunge nane vilivyotokea jana. Mungu alikuwa nasi na akatuokoa. Kuna askari walitupa vitoa machozi na tukapata nafasi ya kutoka kwa hiyo ambulensi. Narudisha shukrani kubwa kwa wale askari ambao walituokoa. Nikiongea juu ya ile Miswada iliyopitishwa, ninasema kuna shida ndani ya nchi hii. Ninashukuru sana kuona Rais wetu akitaka ushuru ulipwe. Kuna bidhaa zingine kama"
}