GET /api/v0.1/hansard/entries/1442432/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442432,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442432/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "ambazo zinatengenezwa huku nchini. Kitu cha kwanza kingeangaliwa ni kama zinaweza tosha kutumika katika miji yote ya Kenya. Jambo la pili ni bei ya sanitarytowels zinazotengenezwa huku ambayo iko juu. Kuna vitu vinafaa kuangaliwa. Ningetaka Wakenya wajue haya mambo muhimu. Ukiwa na mitungi ya maji na imetoboka chini na bado unataka kuweka maji ndani, kitu cha kwanza unafaa kufanya ni kuziba ufa huo. Hilo shimo likizibwa, unaweza kuweka maji. Vile hii sheria imepitishwa, ni kama kuweka maji kwa mtungi uliotoboka. Bw. Spika, unaona watu wanatembea na helikopta, wakiwa na pesa, wakitoa mamilioni kwa michango. Unaona wengine wakienda matembezi nje, Rwanda, Kampala na kwingineko. Mimi nashindwa kuona kwamba watu wengine wanafuja pesa. Ukienda kwa makaunti, asilimia 50 inaliwa. Ukienda kwa Serikali ya Taifa, asilimia 30 inaliwa pia. Ningetaka kumwambia Mheshimiwa Rais awache kuongeza ushuru kwanza na apunguze ukora ambao unafanyika ndani ya hii nchi. Bw. Spika, ukiangalia Serikali ya Taifa, asilimia thelathini inakuliwa na wakora na wanakula pia asilimia 50 kwa kaunti zetu. Tulipitisha Ksh400 bilioni kama mgao wa kaunti. Ukitoa asilimia 50 kutoka kwa hizi pesa, unapata Ksh200 bilioni ndio zimekuliwa. Ukotoa asilimia 30 kutoka kwa Shilingi trilioni tatu, unapata Shilingi bilioni 900 zimeenda. Rais wetu anafanya juhudi usiku na mchana ili nchi yetu ilipe madeni, watu wakae vizuri na shule zinaendelea vizuri, lakini hiyo kazi yote inaharibiwa na wakora. Niki support adjournment, kuna risasi nyingine tulizosikia zamani tukiwa wadogo ambazo zimeweka rubber zinazoitwa, “ rubber bullet ”. Serikali ya Kenya haiwezi kutumia hizo kupiga hawa watoto? Kwa nini wanatumia risasi za kuuwa watu? Mhe. Spika, sijasikia mtu akisema pole kwa wale waliokufa jana. Hata President wa nchi hii hajasema pole. Angeanza kwa kusema pole kwa kupoteza watoto na kwamba hao watoto hawakufaa kufa na hivyo hakutakuwa na vifo vya watoto wengine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}