GET /api/v0.1/hansard/entries/1442697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442697,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442697/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii ili nitoe rambirambi na pole kwa familia ziliopoteza wapenzi wao katika purkushani iliyokuwa katika mji mkuu wa Kenya na viunga vyake na pembe mbalimbali za nchi ya Kenya. Vile vile, nashukuru kwa kujaribu kudhibiti mawimbi katika Seneti. Licha ya kupeana mwelekeo, lazima sisi kama Seneti tujadili kwa kinaga ubaga yale ambayo yanawahusu Wakenya katika awamu hii ya Seneti. Katika Seneti, kuna vitengo na kamati mbalimbali za uongozi. Mara tena na tena, kumekuwa na ripoti zinazoletwa hapa Seneti kuhusiana na ubadhirifu wa pesa za umma, ukabila na mambo mengine ambayo hayaendi sambamba na matarajio ya Wakenya. Sasa tumekuwa hapa karibu miaka miwili na kile najaribu kuwaomba viongozi wa kamati hizi ni kuwa Kaunti ya Garisa imekuwa na changamoto ya ufisadi, kuajiriwa kwa watu pasipo kufuata misingi ya Katiba na kadhalika. Ila Seneti haijachukua msimamo au The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}