GET /api/v0.1/hansard/entries/1442698/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442698,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442698/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "kutoa mwelekeo na makataa ya siku ngapi zinazotarajiwa majibu yatekelezwe na nyenzo mbalimbali za nchi ya Kenya. Naomba Seneti na Bunge la Kitaifa yasipige miayo na kulia pasipo kutekeleza kwa mujibu wa Katiba. Kaunti ya Migori, Trans Nzoia na kaunti zingine mbalimbali zina changamoto ambazo taasisi na kamati hapa Bunge zinajua kuna shida na twajua suluhisho ziko wapi. Naomba kutoka leo, kando na kujieleza na kupeana madawa kama Panadol kwa Wakenya, lazima tupeane matibabu ya kweli kwa wakati unaostahili. Kenya Revenue Authority (KRA) imekuwa ikiajiri watu. Kamati husika ina takwimu za kudhibitishwa lakini bado hatujachukua hatua ya kuwaita waliohusika kuwaajiri watu kinyume cha Katiba ili wang’atuke ofisi zao na taratibu zinazotakikana kufuatwa zifuatwe. Wizara ya Kawi vile vile imewaajiri watu. Hatujaona kamati hizi zikileta ripoti ili viongozi hawa waweze kuajibika. Bw. Spika, naomba kwa sababu Mhe. Rais - kitengo cha walio wengi katika Bunge sasa tunazungumza lugha ya Wakenya, tuweze sasa kuonyesha kwa vitendo kutoka sasa kwenda mbele. Niliposimama hapa ili kujaribu kumwambia Mhe. Osotsi yale yaliyo moyoni mwangu, kile nimegundua vile vile ni kwamba kumekuwa na falsafa ya muungano au"
}