GET /api/v0.1/hansard/entries/1442700/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442700,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442700/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "ambayo imeonekana hapa Kenya. Katika awamu iliyopita, kulikuwa na lawama. Katika awamu hii, tumeona kana kwamba kuna mahaba fulani. Wakati unaostahili, watu wananyamaza. Watu wanapoongea, huenda wako njaa. Wakenya wanauliza haya maswali. Wakati mambo yanafaa kuzungumziwa, watu wananyamaza ndio maana vijana wameamka sasa katika kaunti. Angalia wizara ya vijana katika kaunti zote katika nchi ya Kenya, asilimia 99 sio vijana. Ni mawaziri wanaosimamia vijana katika kaunti zetu. Angalia kazi zinapotangazwa katika kaunti zetu, vijana hawapewi nafasi. Wao ni kuangalia kwenye video na simu za rununu. Kandarasi zinazopewa kitaifa na katika kaunti, vijana hawapewi huku Nairobi wala kule mashinani. Lazima tuonekane tukisema na kutenda. Naomba tuwache kwenda mikutano Mombasa na kadhalika kuandika ripoti za kamati mbalimbali. Tupewe fedha za kutosha tuende mashinani tuchunge pesa tunazopeleka kule."
}