GET /api/v0.1/hansard/entries/1442702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442702,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442702/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Tumekuwa na Kamati ya Ugatuzi kule Bungoma tukiangalia soko. Tumekuwa na Mhe. Osotsi kule Vihiga na Wajir. Tumejionea kwa macho pesa zetu. Wakenya wanapigana kwa sababu hali ya maisha imepanda, wanashtumu Bunge la Kitaifa lakini hapa mashinani katika kaunti, wanakamuliwa pole pole pasipo wao kujua. Sasa sisi tuna mjadala wa public participation . Mahusiano ya Wakenya na viongozi. Tupeleke mchakato huu pale mashinani, wajue bajeti za kauti zinatengenezwa vipi na takwimu za kaunti ziko vipi. Na wao watanufaika vipi kutokana na jasho lao ambalo kwao tunapeleka pesa mashinani? Sasa mimi naungana na Wakenya wote. Juzi, tumeona Waziri wa Elimu na baadhi ya Wabunge katika nchi ya Kenya wakipeana barua za kazi kana kwamba ni barua za watoto kwenda kuleta karo kutoka nyumbani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}