GET /api/v0.1/hansard/entries/1442703/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442703,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442703/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Sehemu zingine, watoto wetu wamepiga foleni kutafuta kazi za ualimu. Kwingine, watoto wanapiga magoti. Wanaponyoosha mikono juu, inawapiga pa kifuani. Tutamkimbilia nani na hawa watoto watamkimbilia nani? Watawalilia nani iwapo baadhi ya wale wanaopeana barua hizi tunawajua? Ni majirani zetu. Ni ndugu zetu. Lakini hatujaona viongozi wakisimama kidete kuwakataza Mawaziri wawache kutumia mbinu za mkato kuwapa watoto wetu kazi ilhali wetu wa mashinani wanajionea kwa macho. Lazima tuseme ukweli. Haijalishi wewe unatoka kabila gani. Cha muhimu tenda wema, nenda zako. Mimi ni miongoni mwa wale vijana chipukizi katika Seneti. Yale ninayoona hapa, wengine wanapiga kelele na kutoa machozi ya mamba. Lakini nyuma ya tent, yale wanayosema na kufanya ni kinyume na yale wanasema katika vipasa sauti. Kutoka sasa kwenda mbele, wacha fisi adhihirike kuwa fisi na kondoo kuwa kondoo ili Wakenya wapate manufaa ya Seneti. Tumekuwa na Kamati ya Kudumu ya Ukulima. Bunge la Kitaifa wameandika ripoti wakatangaza. Sisi Seneti tumetembea pembe mbali tukajionea kwa macho. Mbolea gushi ilitumiwa mfumo upi na wale waliohusika. Leo hii tuko hapa Seneti, ripoti iko wapi? Ripoti iko wapi? Waliotajwa wako Serikalini. Waliohusika, marafiki zao wako hapa. Tuseme ukweli. Tuwache mzaha na Wakenya. Sitaki kupita hapa. Ninataka kuwaambia vijana wa nchi hii, wengi wasifikirie kunyamaza kwetu hatujui. Tunajua. Na sasa vidonda vitafinywa. Ukweli utasemwa. Iwapo uko na kazi yoyote katika kamati yoyote hapa Seneti, fanya kazi yako. Bw. Spika, kuna kamati ambazo zinajadili takwimu na pesa za kaunti na Serikali Kuu. Kila mara tunapokaa hapa, unagundua pale palipo minofu na palipo magavana ambao wako na uzito kidogo. Baadhi yao hawaji hapa. Wako kwingine; wanapanga na kupangua. Ukweli usemwe. Hili donda ndugu lazima tutatue. Wanakandarasi na wafanyibiashara wa kaunti mbalimbali hawajalipwa. Wengine zaidi ya miaka kumi. Magavana hawalipi. Tunapodai hapa walipwe, kuna utepetevu wa kuthibiti na kuhakikisha sheria zinafuatwa na wafanyibiashara walipwe. Kwa nini? Ni kwa sababu baadhi ya viongozi wana mahaba ya kisiasa na magavana na viongozi ili kuwafinya wanyonge hao wapate peremende na waishi maisha yao. Sasa nataka kuona mabadiliko kando na kuzungumza Kizungu ama Kiswahili kizuri. Tunataka kuona mabadiliko kwa vitendo. Kuna sehemu za nchi hii ambazo miundo mbinu ya barabara ni nzuri. Hata barabara zingine, ngo’ombe wanalala wakiota jua. Lakini zingine, wengine wanashangaa wako Kenya gani? Ilhali Mawaziri wa miundo mbinu na barabara wanatembea kwa ndege za kitaifa, simu za bei ya juu, kizungu sijui wamekitoa wapi, ilhali Wakenya wanauliza hata sisi tunatoa ushuru, mbona hatushughulikiwi? Lakini tukiuliza, tunaambiwa nini? Asilimia yako ni ngapi katika Serikali? Kama ni asilimia, siyo utuambie asilimia ya watu wa Mkoa wa Magharibi ni ngapi tulipe. Kama ni asilimia mia moja tulipe ushuru asilimia mia moja. Na jambo la ukabila, tusilifiche hapa. Ukabila ni donda sugu katika Kenya. Watu wawache kusema eti sisi ni nchi moja. Kama wanataka tujadili ukabila, tuweke Hoja Bunge tujadili ukabila. Kama ni uwezo wa kuzaa au kuoa tujadili ili tutatue hili jambo la ukabila. Tumeona juzi kila mtu anasema watu wangu. Kwani nani hana watu? Hata Yesu wa Tongareni ana watu, my friend. Na iwapo Kenya hii lazima isonge mbele, lazima The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}