GET /api/v0.1/hansard/entries/1442717/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442717,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442717/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Natangulia kwa kushukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa na amani kwa taifa letu hadi sisi tukaweza kukaa katika kikao hiki. Pili, ninatuma rambirambi zangu kwa wale waliondokewa na wapenzi wao, watoto wao, waume wao na hata watoto wanaokwenda shule. Kwa hakika, majuma haya mawili ambayo yametupa kisogo hivi sasa, yametutingiza sisi kama jamii na taifa. Bw. Spika, gumzo linaloendelea hivi sasa ni kana kwamba, ugatuzi umeondoka humu nchini. Kwa sababu, anayenyooshewa kidole cha lawama ni Mhe. Rais wa taifa la Kenya peke yake. Itakuwa ni unafiki mkubwa, nisipoangazia suala hili kwa sababu tuko na magatuzi 47 yanayoendeshwa na magavana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}