GET /api/v0.1/hansard/entries/1442718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442718,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442718/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Sisi haswa kama Maseneta ni wasimamizi wa magatuzi haya 47. Lakini, kwa sababu tumeitwa, ni lazima tuitike na tuonyeshe uongozi kwa taifa la Kenya. Sisi kama Maseneta tuko tayari kuziba pengo ambalo limekuwa likiendelea kwa muda mrefu. Bw. Spika, nitaanza na suala la ukabila humu nchini. Nitaendelea na suala la ardhi katika taifa la Kenya. Tunazungumzia maandamano ambayo yameibuka kwa sababu ya suala la Finance Bill . Mimi kama Mhe. Rais William Ruto, nitasema ya kwamba tusiyazungumzie matukio ya majuma haya mawili kana kwamba taifa la Kenya limeanza kupata uhuru wake. Nitazungumzia suala la ufisadi. Kwa sababu, baada ya mengi tuliyoyazungumzia, ya kwamba, hatutaki mapendekezo ya kutoshwa ushuru yaliyopelekwa katika Bunge la Taifa---"
}