GET /api/v0.1/hansard/entries/1442722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442722,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442722/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Kumekuwa na malimbikizi ya matatizo ambayo yamesonga mawazo yetu humu nchini. Kule Mombasani, Gatuzi 001, na sitaongea hapa kama kiongozi wa kitaifa ikiwa nitajitoa kama kiongozi ambaye ametoka nyanjani. Ninamshukuru Mhe. Rais kwa kunipa fursa hii kwa sababu chama cha UDA kilitafuta vijana wakakamavu. Tunapozungumzia Gen Z, hata sisi kina Miraj ni Gen Z wa kutoka kule 001. Kwa sababu tumesema tutazungumza bila unafiki, niruhusu kusema haya, kule Mombasa, tumekuwa na tatizo la ardhi. Familia zetu zimepewa barua na naomba nitaje vitongoji, pale Bondeni, Mwembe Kuku, Likoni Visangalaweni, Tudor, Kisauni na maeneo yote. Haya yote yanakuja kwa sababu taasisi zinapopeana recommendations, hakuna kitu kinafanyika. Sisi kama Serikali ya UDA, tulizunguka katika taifa la Kenya na tukawaambia Wakenya ya kwamba, kuna makosa yaliyotendeka wakati wa Serikali iliyopita. Lakini, tangu tuingie mamlakani, hakuna hata mtu mmoja amewekwa pingu katika mikono yake kuashiria yale tuliyokuwa tunazungumzia wakati wa kampeni tumekuja kuwafanyia wananchi wa Kenya haki. Bi. Spika wa Muda, nikibaki katika nukuu yangu ya maswala ya mashamba, jambo la kusikitisha ni kwamba, mawakili wanaowasimamia wale wanaotunyanyasa sisi, ni miongoni mwa viongozi wanaokwenda kuzima nyota ya jamii zetu waliopokonywa mashamba yale. Nikisimama katika nukuu ya ufisadi, ningependa kuzungumzia taasisi kama ya EACC, ni jambo la kusikitisha. Tungependa taasisi hizi ziweke wazi. Je, wale wanaoondelewa mashtaka hivi sasa, walikuwa wameshitakiwa kwa uonevu ama ni kwa sababu, saa hizi wako sawa kisiasa ndio maana taasisi hii inakunja mkia na kuwaachilia huru bila haki kupatiwa wananchi wa Kenya? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}