GET /api/v0.1/hansard/entries/1442723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442723/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, nimezungumzia mambo ya malimbikizi ya hasira yaliyowafanya vijana wetu kwenda barabarani. Nilizungumza katika Bunge hili kuhusu kufunguliwa kwa anga ya Moi International Airport. Cha kusikitisha ni kwamba, Waziri alifungulia ndege moja ya Kenya Airways kutua na kwenda Dubai. Lakini, niliposimama hapa, niliomba Bunge hili la Seneti liweze kufungua anga kwa ajili ya ndege zote ili utalii uweze kushamiri katika majimbo yetu. Hakuna mtu mwenye njaa aliye na furaha. Watoto waliokuwa katika barabara zetu wa Gen Z walikuwa wameumia kwa muda mrefu sana. Hii ni kwa sababu hawapati fursa sawia. Ninazungumza kwa nukuu ya mtoto wa Pwani ambaye anasikia kuna walimu 50,000 walioajiriwa na Serikali ya Kenya. Lakini akiulizwa ni mwalimu gani ameajiriwa, hawezi kusema ni nani ameajiriwa. Haya ndio miongoni mwa masuala tata yaliyofanya vijana wetu kwenda katika barabara. Baada ya Jiji la Nairobi, jiji au gatuzi iliyofuatilia kwa wingi wa watu waliojitokeza ilikuwa Gatuzi 001. Nazungumza kwa uchungu kwa sababu, hata wale vijana wetu tunaowapeleka kwenda kusoma pale Bandari Maritime Academy, zile shahada wanazopewa haziwaruhusu wao kuingia meli za kitaifa. Hii ina maana kwamba hizo shahada hazifikii viwango vya kitaifa. Mtoto anasoma pale, anarudi anaingia kwenye meli na anawaambia aende South Africa aende akasome tena. Nilikuwa nimepata chemichemi ya furaha lakini naona ndoto yangu ilizimwa kwa sababu Finance Bill haikupita. Bi. Spika wa Muda, kama walivyotangulia kusema viongozi wenzangu, ninamwomba Mhe. Rais wangu kipenzi, aweze kulivunja Baraza la Mawaziri haraka iwezekanavyo. Haiwezekani yale mazuri ambayo mtoto wa Pwani alikuwa anaenda kuyapata katika hii Finance Bill ameyakosa kwa sababu kuna mtu hakutoka akajieleza vizuri. Ningependa kuwapongeza Wabunge wenzangu tuliokuwa nao kule Ikulu ya Rais. Nimeambiwa mimi, Miraj, msimamo wako mkali kusimama nyuma ya Rais utakufanya usichaguliwe. Nitatumia fursa hii kuwaeleza vijana wa Kenya ya kwamba ile Finance Bill walioikataa na wakaamua haitakuwa sababu ya wao kupasua kile kilichoko ndani, wamepoteza mambo mengi mazuri sana. Bi. Spika wa Muda, ninawapigia saluti Wabunge wenzangu nikianza na Mhe. Ruweda aliyekejeliwa na kukashifiwa kwa sababu hawakufanya makosa. Ilikuwa muhimu kwa taifa na kwa Mhe. Rais kukataa kutia sahihi Mswada wa Fedha. Siyo Mswada ulikuwa mbaya, bali tuna mazungumzo mengi kama taifa ambayo tulipaswa kuyazungumzia. Nafurahi kwamba leo nimeweza kusimama hapa watu wanapozungumzia uporaji wa raslimali. Nashangaa jinsi viongozi wanavyoongea. Kinachoniumiza ni kwamba, pale Mombasa, ni miaka kumi tangu ugatuzi uanze, lakini hatuna uwanja wa kucheza kabumbu ambapo wa pwani walikuwa wanasifika kwa kuweza kuisakata. Uwanja huu wa Mombasa mpaka leo umebaki kuwa ndoto kwa sababu ya ufisadi. Mamilioni ya pesa yaliekezwa lakini Mombasa Stadium imekuwa shamba la wanyama. Ukingia pale, unapatana hata na simba ilhali mamilioni ya pesa yalitengwa. Nashangaa wanaposema kuwa Mhe. Rais ni wakutenga. Watu wa Mombasa, nawaomba mniangalie kwenye macho yangu na mnieleze na tukubaliane ni mamilioni mangapi yametengewa Mombasa na yameibiwa. Ikiwa tunataka kuinyorosha nchi hii na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}