GET /api/v0.1/hansard/entries/1442724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442724,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442724/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwa wa kweli na uongozi wa taifa la Kenya, tuwe wa kweli kuanzia pale tulipo. Tuliamka na tukapigia kura sita lakini kidole cha lawama kimebaki kwenye kura moja. Namwambia Mhe. Rais William Samoei Ruto kwamba ukubwa ni jaa. Kubali kila kitu unachotupiwa. Kwa kauli yako katika maswali uliyokuwa unatupiwa na waandishi wa habari, ulisema umefurahi kuwa vijana wametufikisha hapa. Huu ndio wakati tuache kujificha nyuma ya microphone . Kila mtu katika Bunge hili yuko na jukumu la kuweza kulinda raslimali ya Mkenya. Sisi sote tuko na jukumu la kuhakikisha kwamba yale mapendekezo tunayopeana kama Bunge yanasikilizwa. Bi. Spika wa Muda, hii Seneti iliuamua ya kwamba wanaoishi Pakstani Point warejeshwe katika nyumba zilizojengwa za Affordable Housing . Lakini mpaka leo, baada ya ripoti kuandikwa na kuidhinishwa na Seneti, hakuna mtu yoyote aliyekuwa mkazi wa Pakstani Point aliyerejeshwa kukaa katika nyumba hizo. Ni jambo la kusikitisha kwamba tume ya Inte-Governmental Relations Technical Commission (IGTRC) ilitengezwa katika taifa la Kenya, ripoti ikaandikwa na mapendekezwo kutolewa. Lakini mpaka sasa, ripoti hizi ama madaftari haya yamebaki katika shelves za Bunge hili. Hakuna hata moja iliyotekelezwa. Ikiwa kweli tuko tayari kubadilisha mienendo yetu, tuache unafiki wa uongozi wa kunyosheana vidole vya lawama. Nilisikia Seneta mmoja akisema kwamba watu wata resign . Chakushangaza sijiaona Seneta yeyote ame resig n. Katika Bunge hili, tuna kamati zinazosimamia raslimali hizi. Nimezungumzia baadhi ya mipango iliyopangwa na magavana ambao leo hawako mamlakani na miradi haikufanyika. Je, lawama hii pia tutamtwika Mhe. Rais? Nakumbuka wakati wa campaign tukisema ya kwamba Ksh2 bilioni zilikuwa zinapotea kila siku. Lakini mpaka sasa, hakuna mtu hata mmoja aliyevishwa pingu na tukaambiwa huyu ndiye aliyekuwa sababu ya kupotea kwa mabilioni yale ya pesa. Je, sisi kama viongozi tunawaambia nini wale walioko nje? Bi. Spika wa Muda, nashukuru kwamba leo Kiongozi wa Waliowengi, ametupa fursa tuyatoe yaliyomo mioyoni mwetu. Tunasikitika kwa sababu Mhe. Rais alizunguka na akatutafuta sisi tuliokuwa kule mashinani tukizungumzia masuala ya mashinani lakini tunashindwa kuona tatizo liko wapi. Nimesikia Mhe. Rais kwa kauli yake akituambia ya kwamba, alipoingia katika uongozi, aliweka sahihi na akapeana independency kwenye polisi. Leo hii, bado kuna mtu anamuuliza Mhe. Rais kwa nini watoto wameuliwa. Ndiyo maana narudia kusema, ukubwa ni jaa. Taasisi zote zifanye kazi zilizowekewa kufanya. Sio kama viongozi, kila saa kunyosheana vidole kwa sababu tunautaka ufuasi wa wakisiasa. Bi. Spika wa Muda, ni miaka 12 tangu ugatuzi. Watu wa pwani wamekuwa wakipewa mabilioni ya pesa lakini mpaka sasa, sisi watu wa pwani tunasema, “ we aremarginalized ”. Nataka kujua fedha zile zinaenda wapi. Mbona hatusikii nduru katika magatuzi ambayo yamekuwa yakisema yako marginalized . Ni shida gani tuko nazo kama wananchi? Bi. Spika wa Muda, hatua kali zichukuliwe kwa maafisa waliotumia nguvu katika maandamano haya. Naomba maafisa wote waliotumia nguvu hadi kuangamiza maisha ya watoto wetu wachukuliwe hatua bila kusaza wale wananchi walioonekana bayana wakiwapiga maaskari wetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}