GET /api/v0.1/hansard/entries/1442731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442731,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442731/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, vifo vyao vitakumbukwa kwa muda mrefu katika historia ya nchi yetu ya Kenya. Vile vile, natoa salamu kwa wale waliojeruhiwa na kupoteza mali zao kutokana na vurugu zinazoendelea katika nchi yetu kutokana na maandamano yaliyoongozwa na Gen Z. Pia, natambua udhamini wa Hoja hii iliyofanywa na viongozi wa walio wengi na wachache wa Bunge hili. Imeweza kuleta shwari katika nchi yetu na Bunge hili kwa sababu watu wamepewa fursa ya kuzungumza yote yaliyomo mioyoni mwao. Kenya ni moja na ndio nchi ambayo sote tunaipenda. Hatuna mahali pengine pa kuenda. Ni masikitiko makubwa kwa nchi yetu kwamba maandamano yalikandamizwa kwa matumizi ya nguvu za kupita kiasi. Tumeona maandamano ya juzi yalivyozimwa pamoja na yale ya mwaka jana yaliyofanywa na wafuasi wa Azimio la Umoja. Kuna muelekeo ambao siyo sawa kwa polisi wetu. Hii imetokana na kwamba polisi wetu hawajaweza kusoma Katiba inavyoamrisha. Katiba inatupa fursa ya kuandamana kwa amani. Tuliona wale vijana waliojitokeza waliandamana kwa amani, isipokuwa maandamano yale yalifurushwa na polisi kwa njia isiyokuwa ya sawa. Nachukua fursa hii pia kuwapongeza vijana wetu wa Gen Z kwa kuweza kuidhibitishia nchi kwamba wanaweza kuwa na umoja, kupambana na ukabila na pia kuleta siasa za maoni ama issues kuliko zile siasa za kikabila na kimbari."
}