GET /api/v0.1/hansard/entries/1442741/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442741,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442741/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, matatizo ambayo yametukumba ni malumbukizi ya matatizo yaliyoanza wakati wa uhuru. Wakoloni walipoondoka, waliingia wakoloni mamboleo ambao wameendelea kutugandamiza mpaka hivi sasa. Ugandamizi huu uko katika hali ya kudhibiti rasilmali za nchi. Tunaona ya kwamba rasilmali za nchi zinadhibitiwa na wachache na wengi wetu wako katika ligi ya umaskini na uchochole kwa muda wote huu. Tulielezwa kwamba Kenya ni kampuni ambayo ina wanahisa. Wengine kama Sen. Cherarkey hapa ni wenyehisa ndio sababu anazungumuza wakati mimi ninazungumza. Gen Z wametuonyesha kwamba hao ndio wenyehisa katika nchi hii ya Kenya. Wao ndio walisema kwamba watakuja Bunge na walikuja Bunge. Ni jambo la kusikitisha kwamba Bunge pia halina uongozi. Hatuna uongozi katika Bunge hili na pia kwenye Bunge la Kitaifa. Tuna wenyeviti ambao wanasimamia mijadala katika Bunge hizi. Ilikuwa vipi Mwenyekiti ama Spika wa Bunge la Kitaifa kukosa kuwasiliana na wale waliokuwa wanaleta maandamano na akapokea memorandum yao hapa nje? Tulikosa vipi sisi viongozi wa Bunge hili la Seneti kujitolea kuenda kusimama pale nje na kuweza kupokea memorandum ambayo iliyokuwa inaletwa na Gen Z?"
}