GET /api/v0.1/hansard/entries/1442743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442743/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Dada yangu, Sen. Mumma, anasema kuwa alienda. Mara nyingi tumeweza kupokea memorandum kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamezileta katika Bunge hili. Matokeo ya juzi, Jumanne, yalikuwa ni doa katika Bunge hili. Bunge hili huwakilisha wananchi. Wananchi walikuwa wanakuja hapa kuonana na viongozi wao. Lakini sisi viongozi tulikimbia na kuwaacha wapigwe risasi. Ni makosa wananchi kuuliwa mbele ya Bunge lao. Hata katika zile nchi ambazo maandamano yanaendelea, kwa mfano, Israeli, yameendelea kwa muda zaidi ya miezi sita lakini hakuna watu wameuliwa nje ya Bunge lao. Bi Spika wa Muda, tukizungumzia mambo ambayo yako hapa, ufisadi ni kidonda sugu katika taifa letu. Tume ya ufisadi imekuwa kwa zaidi ya miaka 10 lakini hakujakuwa na mafanikio yoyote katika kupambana na ufisadi. Vita dhidi ya ufisadi vinapigwa kisiasa. Kama hauko katika mrengo wa Serikali ambayo iko mamlakani huwezi kuepuka kupelekwa mahakamani. Unapata kuwa wengi wanaohutumiwa na Tume ya ufisadi wanajisongesha karibu na Serikali iliyoko mamlakani ili waondolewe mashtaka na lawama ya mambo ya ufisadi. Ufisadi umeingia pia katika Bunge hili letu. Ndio maana kama alivyozungumza Sen. Osotsi, kabla ya kupiga kura ya Mswada muhimu huwa tunaitwa Ikulu kuenda The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}