GET /api/v0.1/hansard/entries/1442744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442744/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "kuzungumza juu ya huo Mswada. Tunatoka pale na bahasha kama zile zinazotoka kwa viongozi wa kanisa. Ufisadi huu ndio umetufanya sisi kudharauliwa mpaka na watoto wetu ndio sababu waliandamana hivi juzi. Mahakama pia zimelemewa. Wiki mbili zilizopita hakimu mmoja alipigwa risasi ndani ya mahakama hapa Nairobi, upande wa Makadara. Ijapokuwa tulisema tukio hilo lilikuwa jambo la kipekee, lakini ilikuwa shutuma kubwa kwa taasisi zetu za kitaifa. Itakuwaje hakimu anapigwa risasi ndani ya mahakama? Huyo alikuwa hakimu ambaye anatekeleza majukumu yake kama sheria inavyomuamuru lakini anapigwa risasi ndani ya mahakama na afisa mkubwa wa polisi. Bi Spika wa Muda, tukio hilo halikuangaziwa kikamilifu. Tuliipitisha hivi na vile kienyeji lakini ilikuwa doa kuu kwa taasisi zetu za kitaifa. Wale walipokuja hapa Bungeni walikuwa wanaendeleza zile shutma ambazo wako nazo kwa taasisi za kitaifa ikiwemo pia Bunge ambayo iliingia katikati. Tumeona jela zetu zimejaa na vijana wadogo ambao wamewekwa pale labda kwa sababu ya kushindwa kufadhili bond za kuwatoa nje. Tukitemebea jela zote utapata zaidi ya asilimia kubwa ya walio huko ndani ni wale ambao wameshindwa kutoa bond ."
}