GET /api/v0.1/hansard/entries/1442747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442747,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442747/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi Spika Wa Muda, mahakama zetu zimejaa vijana wengi ambao wameshindwa kudhibiti masharti ya bond ambayo inatolewa na mahakama zetu. Bond zinazowekwa na mahakama zetu ziko juu kiasi ambacho yule anayetakikana kulipa anashindwa kwa sababu hata labda kwake hana chakula cha kula. Jana, kuna mshatikwa mmoja kule Eldoret ambaye alipewa bond ya shilingi 10 milioni kwa kosa la kuiba kilo 181 za nyama. Tukiangalia bond hizo na za wale ambao wanashtakiwa makosa makubwa, hazifanani kabisa. Juzi, yule mtumwa wa ile scandal ya Triton ambaye alitumiwa kuiba zaidi ya shilingi 10 trillioni alipewa bond ya shilingi milioni moja, akatoweka na mpaka sasa hajapatikana. Mahakama zetu zimeingia katika ligi ya ufisadi na utepetevu kiasi ambacho kupata haki katika mahakama hizi imekuwa shida. Wananchi wanatafuta njia mbadala za kutatua matatizo yao. Kutoka mzozo huu kuanza, Serikali ya Kenya Kwanza imekuwa na vichwa viwili. Juzi tulimwona Mhe. Rais William Ruto akitoa taarifa yake 4.00 p.m. na baadaye Naibu wa Rais akatoa taarifa yake 5.00 p.m. Katika hali kama hii sio sawa viongozi wawili wakuu katika Serikali kuonyesha sura mbili tofauti. Sisi tunajua Serikali ni moja na kichwa ni kimoja. Mambo yaliyotokea juzi yalionyesha kuwa kuna vichwa viwili katika Serikali hii. Tunaona pia kuwa Baraza la Mawaziri limekuwa kimya. Hakuna Waziri ambaye anazungumza chochote kuhusiana na michafuko inayoendelea katika nchi yetu hivi sasa. Bi Spika wa Muda, tunataka Serikali izungumze na sauti moja kwa sababu Serikali ni moja na kiongozi wake ni mmoja. Kama wanataka kuwa na Serikali mbili, basi wakafanye vile nchi nyingine hufanya. Lakini hapa kwetu tunapendelea Serikali iwe moja. Tumeona pia masuala ya extrajudicial killings bado yanaendelea ijapokuwa Serikali hii ilipochaguliwa, walisema jambo hili litawekwa katika kaburi la sahau. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}