GET /api/v0.1/hansard/entries/1442748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442748,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442748/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tumeona juzi hapa nje ya Bunge zaidi ya watu wanane walipigwa risasi na kupoteza maisha yao. Kuna baadhi ya wale wanaofuatwa usiku majumbani mwao na kutekwaa nyara bila ya kujulikana wanaenda wapi. Hii sio Serikali ambayo ilichaguliwa na Wakenya. Hata kukamata mtu inakuwa ni vita. Juzi, tuliona mbunge wa zamani, Mhe. Alfred Keter, akitoka kanisani na kutekwa nyara kama mhalifu. Hio sio nchi ya kistaarabu. Kama ni kweli, tume hiyo inafaa ichunguze. Wanafaa kumwita na akikosa kwenda, wachukue warrant ya kumtaka ili aende ajibu mashtaka. Tukiangazia suala la ukosefu wa kazi, Serikali inasema kwamba inapeleka watu Saudi Arabia, Dubai, Qatar na Marekani lakini kupata pasipoti ni shida kwa sababu inachukua miezi sita au zaidi. Watu wetu wanaambiwa kwamba watapatiwa kazi katika nchi za nje. Wanaambiwa kuwa watapewa kazi kule Marekani, Uchina, Ujerumani na kwingineko lakini kupata pasipoti ni shida katika nchi yetu ya Kenya. Vijana ambao tunaahidi kazi za nje watakwenda vipi. Zamani katika Halmashauri ya Bandari, kulikuwa na vibarua waliokuwa wanachukuliwa kwa kile kilichojulikana kama “ White Card ”. Baada ya muda, walikuwa wanafuzu na kupewa kazi za kudumu. Mpango huo wa “ White Card ” uliondolewa na sasa zabuni zinatolewa kwa watu binafsi kupeleka watu kufanya kazi bandarini. Watu hao wakipewa kazi zile, watanyanyasa wafanyakazi ambao hawatapata haki zao kikamilifu. Vile vile, utendakazi utazidi kudorora katika bandari ile. Tunashutumiwa na mashirika ya kimataifa kama International Monetary Fund (IMF) kwamba tunafaa kupunguza wage bill na wafanyikazi lakini ukiangalia, nchi yetu inaendelea. Ilivyokuwa Bandari ya Mombasa miaka 20 iliyopita sio ilivyo sasa lakini wafanyikazi wanazidi kupungua. Uekezaji katika mashirika yetu hautusaidii sisi kama Wakenya kwa sababu watoto wetu hawawezi kuajiriwa kazi ilhali tunatoa ardhi na kodi kufadhili mashirika yale. Ikiwa hawawezi kupata kazi, vijana wetu wataajiriwa wapi? Tunataka waende waajiriwe katika bandari za Dubai au Rotterdam wakati tuna Bandari ya Mombasa? Mambo hayo lazima yaangaliwe. Hatuwezi kupambana na ukosefu wa kazi ikiwa hatutakuwa wabunifu. Leo hii, kuajiri watu Mombasa kutumia “ White Card ” ni rahisi kuliko kuwapeleka Dubai kwa kazi ambazo hazijulikani halafu tunalalamika kuwa wafanyikazi wetu wananyanyaswa katika nchi za nje wakati mila na desturi zetu ni tofauti na kule ugenini ambako wanaenda kufanya kazi. Tumesema kwamba tutoe mapendekezo. Nakubaliana na wenzangu waliosema kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi anafaa kujiuzulu. Jana kulikuwa na maandamano kule Mombasa na ofisi zetu zililengwa mawe na waandamanaji. Ofisi yangu kule Mombasa ililengwa mawe na gari la mtoto wangu likachomwa. Polisi walikuwa wamekaa tu wakiangalia. Polisi walikuwa wakati magari yalikuwa yanachomwa. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo hatungependa kushuhudia tena katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu hakuna kosa ambalo tulikuwa tumefanya katika ofisi ile wala hakuna shinikizo lolote ambalo tuliambiwa tufanye tukakataa. Tunaposema kuwa Bw. Koome ambaye ni Inspekta Jenerali wa Polisi amepoteza mwelekeo, tunamaanisha kuwa hajawaeleza kikamilifu mambo ambayo polisi ambao anawasimamia wanafaa kufanya. Wanaposema kuwa mahakama iliwazuia, huo siyo ukweli. Mahakama ilisema kuwa wasitumie silaha wakati mali na maisha ya watu yamo hatarini. Iliwazuia kutumia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}