GET /api/v0.1/hansard/entries/1442749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442749,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442749/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "silaha bila mpango. Wakati mwingine unapata kuwa wananchi wanaandamana kwa amani ilhali wao wanatumia vitoa machozi au kufyatua risasi ili kuwadhuru wandamanaji. Mwisho, kuna wale ambao wameshtakiwa kwa makosa madogo madogo kama vile kushiriki maandamano au kusema “ Ruto must go .” Hayo siyo mashtaka ya kupeleka mtu mahakamani. Serikali inafaa kuondoa mashtaka hayo na kuhukumu wale ambao wametuhumiwa kwa ufisadi ili turejeshe pesa walizochukuwa ili kusaidia Wakenya kupata ajira, huduma za afya na kusomesha watoto wao. Kuna pendekezo la kuwaita Wabunge kutoka likizo ili kujadili upya mapendekezo ya kuondoa Mswada wa Fedha wa 2024. Naunga mkono pendekezo hilo kwamba lazima Wabunge waitwe. Mswada huo ukitoka katika Bunge la Taifa, lazima pia uletwe katika Seneti kwa sababu unahusu masuala ya fedha ambayo yanaathiri tume huru. Kwa hiyo, unafaa kuletwa katika Seneti kulingana na Katiba. Kwa kumalizia, masuala ya ukabila yamekithiri katika kaunti zetu zote. Isipokuwa katika kaunti za Nairobi na Mombasa, ukienda katika kaunti zingine katika Jamhuri ya Kenya, utapata kwamba asilimia 98 ya wafanyikazi wanatoka katika kaunti hizo. Tuna Kamati ya Mshikamano wa Kitaifa, Fursa Sawa na Utangamano wa Kikanda lakini haijakwenda katika kila kaunti kuangalia masuala hayo. Hatuwezi kuzungumzia umoja wa kitaifa ikiwa tunazungumzia mambo ya ukabila au mbari katika kaunti zetu. Utapata watu wanasema kuwa anayefaa kupata kazi katika kaunti zetu anafaa kutoka mbari hii au ile. Kama tunataka umoja wa kitaifa, ni lazima tukubaliane kwamba kuajiri watu katika sekta za umma lazima kuwe sawa katika kila sehemu. Kila mwaka, vijana wanachukuliwa kujiunga na vikosi vya majeshi."
}