GET /api/v0.1/hansard/entries/1442752/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442752,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442752/?format=api",
"text_counter": 160,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Hata hivyo, kaunti zingine hupata nafasi zaidi kuliko zingine. Katika kila eneo bunge, vijana huchukuliwa kujiunga na vikosi vya askari na majeshi. Ukiangalia kwa makini, maeneo bunge mengine hupewa nafasi ya watu 10. Mengine hupewa nafasi ya watu 20 na mengine mtu mmoja tu. Inakuwa vipi ilhali kila eneo bunge linafaa kuajiri watu sawa? Ni muhimu kubuni kamati katika Seneti kujadili mambo haya. Inatakikana tutoe mwelekeo kwa haraka zaidi kuliko jinsi ambavyo mambo yameweza kufanywa. Hiyo ndio sababu wengine tulikataa Maseneta kwenda likizo ili tujadili maswala haya kikamilifu na kutoa mwelekeo. Leo wananchi wengi wamepiga simu kutuunga mkono kwa hatua ambayo tumechukua ili kuweka mambo wazi bila ya usumbufu wowote---"
}