GET /api/v0.1/hansard/entries/1442783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442783,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442783/?format=api",
"text_counter": 191,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ukiwa miongoni mwa watu wa mwisho kuzungumza, mara nyingi unapata kuwa mambo yote yamesemwa. Hata hivyo, sisi waliokula chumvi nyingi hatukosi maneno ya kuongezea. Bi. Spika wa Muda, nashukuru kwa kupewa nafasi hii. Kwanza kabisa, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wale waliofiwa na wazazi ambao watoto wao wako hospitalini. Tunawaombea Mungu awape subira kwa kupoteza watoto wao. Hakuna kitu kibaya kama mzazi kumpoteza mtoto. Hakuna uchungu mkubwa kuliko mtoto kutangulia kuaga. Nachukua nafasi hii pia kushukuru kwa mambo mazuri ambayo tumesikia kutoka kwa the Senate Majority Leader, Sen. Cheruiyot, the Senate Minority Leader ambaye ni mkubwa wangu, Sen. Madzayo, pamoja na Secretary General (SG) wa chama changu. Kusema kweli yale ambayo mmesema ni mazito sana na singetaka kufanya yawe mepesi. Mmesema na Wakenya wamesikia. Wazazi haswa sisi kina mama tunahisi uchungu sana kuona watoto wetu wakiuawa huku tukiangalia wakati wao hawana silaha zozote. Watoto wetu wametekwa nyara. Hiyo inatufanya kuendelea kulia. Kusema kweli, nitaongoza wanawake wajitokeze kuunga mkono watoto wetu, ili nasi pia tuuawe kwa kuwa wanatendewa unyama."
}