GET /api/v0.1/hansard/entries/1442791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442791,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442791/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Kwa mambo ya kazi, vijana wanaomba wapewe kazi. Kulikuwa na shida KRA ambapo tuliona application ya makabila mawili, hadi watu wakaenda kortini. Huko kwenda kortini, korti imesema kwamba haina nguvu lakini inakubali kwamba kabila zilikuwa mbili. Kusema kweli, hiyo ingekuwa ni pigo kubwa kwa Mhe. Rais na papo hapo, angechukua hiyo nafasi ya kuweza kubadilisha mambo mengine, lakini alinyamaza. Hata alipoambiwa kwamba alisafiri kifahari, bado alishindana hadi Wakenya wakatoa ukweli kuwa Kenya Airways (KQ) ilikuwa ni nauli ya chini kuliko vile yeye alisafiri. Kwa hivyo, mambo mengi yamejitokeza lakini uzuri ni kuwa, tumeanza kukubaliana kwa sasa. Watu wazima huzima, hawawashi. Kwa hivyo, Seneti ni watu wazima, tujaribu kuzima. Kusema kweli, haitatusaidia na chochote tukiwasha. Bi. Spika wa Muda, nimefanya kazi na Umoja wa Mataifa na nimekuwa Sierra Leone, Afghanistan na nchi zingine. Kusema ukweli, nimeona maisha ya Sierra Leona watu wakiulizwa wachague kama wakatwe mkono short or long sleeve ama mguu kwa sababu lazima watakatwa. Kusema kweli, nimeona vile maisha ya huko yalivyokuwa na mpaka leo hayajarudi kawaida. Leo, hatuwezi nchi yetu iwe hivyo. Katika mwaka wa 2007, tuliona kidogo tu na hadi leo, tuko na Internally Displaced Persons (IDPs) ambao hawajarudi kwao kwa sababu ya maafa kama hayo. Kwa hivyo, tunaomba wale wako karibu na Mhe. Rais waweze kumwambia kuwa huku nje ni kubaya, kwa hivyo asikize. Mhe. Rais mwenyewe alikuwa anaambiwa mtoto amepigwa risasi nane na bado anauliza kama huyo mtoto alifariki. Kusema kweli, inaonekana kuwa hamna mtu yuko karibu na Mhe. Rais. Bi Spika wa Muda, jana niliona uchungu sana. Kijana alikuwa amebeba bango linasema- “Mama Rachel, mtilie Rais sumu afe, Kenya iwe huru”. Nafikiria wengine wenu wote mliona. Sen. Madzayo, nilikuonyesha. Jamani, imefika hapo? Wazazi wanalaani nakusema kwamba wamemlaani Mhe. Rais akiwa kwenye ndege nayo ndege ianguke afe. Huo ni uchungu wa mzazi. Na leo, mimi nazungumza kama mzazi na mama. Labda hivi Karibuni, pia nitakuwa na wajukuu."
}