GET /api/v0.1/hansard/entries/1442793/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442793,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442793/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "leo mtoto wangu awache wajukuuu wangu ambao ni watoto wake bila baba wala mama, maanake wote wamehusika. Hii haikuwa ni mtoto wa tajiri wala maskini, mtoto wako na wangu waliweza kutoka. Watoto waliuliwa kinyama walikuwa na simu zao tu na bendera ya Kenya wakisema sisi ni Wakenya. Imagine unyama wale wale polisi ambao walikuwa wanawatetea, wanawauwa watoto kinyama? Halafu jana, vijina wanaotetewa hawawezi kuwadhulumu. Wamesingiziwa kuwadhulumu. Kusema ukweli, leo tunakubali Mhe. Rais, kesho mambo ni mengine. Kutaka kujua bado nchi haiko sawa, Mhe. Rais na Makamu wake wameanza kushambuliana. Mhe. Rais anazungumza hivi, Makamu wake anazungumza vile. Mhe. Rais anasema, Majority Leader wangu au Secretary General wangu akishazungumza siwezi kuzungumza bila kupewa nafasi. Lakini, itakuwaje Mhe. Rais anazungumza mengine na Makamu wake mengine? Inaonekana tofauti zimeanza. Nyumba ikiwa haijakaa sawa kwa hao wawili, mume na mke, kwa mfano, watoto watakaa vipi? Hapa mambo ni mengi sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}