GET /api/v0.1/hansard/entries/1442798/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442798,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442798/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "ila ukiifungua hakuna kitu, ni hewa ilhali kuna watu wanalipwa. Watoto wetu wale wanasomea utabibu na udaktari, juzi walisema, ‘jameni, tusaidieni, tunaomba tu kitu kidogo.’ Lakini leo, Katibu Mkuu wetu amesema kuwa kwenye gari lake tu, ameekewa fedha ngapi ya kupita Nairobi Expressway? Kusema kweli, Kenya kuna vitu vingi sana vimeanguka. Mhe. Rais umeambiwa hicho kikoi chako kiko wazi. Utafanya nini? Kubali useme ni hivi na vile na mimi niko tayari. Tumeona kwa runinga Mhe. Rais unaambiwa shida iko hapa, lakini bado kuna utatanishi fulani. Mimi naomba tuwe na vikao kutoka Seneti na Bunge la Kitaifa. Sote tukae chini tuone ni njia gani tutaweza kuwasaidia hawa vijana wakubwa. Tunaambiwa ukubwa ni jaa. Jaa ni kuwa na shida zote. Kuna zile ambazo Seneti hii inapaswa kuzibeba. Hizo dakika kumi naona zilikuwa kidogo. Mambo ni mengi na pia mazito. Lakini mimi nitalia tu. Jambo la mwisho, kama mama, tuangalie vijana wetu. Na jambo hili la vifo likome. Hili jambo la kuuwa vijana wetu likome. Kama kesho wanataka kutoka nje kwenda kuzungumza na watu, wacha waende. Wapewe nafasi. Msiweke wezi tena wadhulumu watoto wetu. Wanaodhulumiwa zaidi ni wasichana wetu. Hivyo basi, hii ni nafasi kubwa ambayo tumepewa kama Seneti The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}