GET /api/v0.1/hansard/entries/1442799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442799,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442799/?format=api",
    "text_counter": 207,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "ya kukubali makosa yetu. Tunaomba msamaha kwa Kenya kama kwa njia yoyote ile tumewakwaza Wakenya na vijana wetu. Lakini Mhe. Rais ndiye anafaa kutoka nje na yeye kwa kuwa kurudisha ule Mswada sio kuukubali. Ahakikishe kila kitu kimerudishwa na Bunge la Kitaifa limekaa chini na kurekebisha kila kitu. Naona muda wangu ni mdogo. Nikianzisha chochote kile, hatutaweza kumaliza. Mwisho basi namuelezea Mhe. Rais ya kwamba mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu mchungu. Ujue hii damu ya wale watoto itakudhuru wewe na watoto wako na vizazi vyako. Kama leo huwezi kutoka nje na kukubali kila na kuomba msamaha wale watu wamefiwa, leo ujue machozi ya Wakenya yatakuumiza. Kama sio wewe, vizazi vyako. Na hii nafasi ya Mhe. Rais ujue ni ya miaka mitano au kumi. Ujue utarudi kwa maisha ya kawaida na familia yako pia. Mkirudi kwa maisha ya kawaida, utakaa wapi? Ni Kenya utakaa ama kwingine kwa sababu unaelewa vile mambo yatakuwa. Kwa hivyo, leo usifanye mambo ukijisahau. Na sisi pia kama Seneti tusijisahau kuwa hata sisi kesho tutatoka na wengine watachukua hii nafasi. Sisi tuko tayari kama Seneti. Mimi najitolea kwa dhati iwapo kutakuwa na maridhiano kusaidia. Tujaribu kuzungumza ile lugha inayofaa isiyo na utatanishi. Kwa sisi watu wazima, tunazima, hatuwashi. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}