GET /api/v0.1/hansard/entries/1442869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1442869,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442869/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza naunga mkono Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu imekuja wakati unaofaa. Leo nasimama hapa Seneti nikiwa na majonzi mengi sana kama Bunge la Seneti kwa sababu kufikia sasa, Kenya imepoteza maisha ya watu 39. Vile vile, ukiangalia katika hospitali zetu zote Kenya, na sekta mbali mbali kuanzia baharini hadi Lake Victoria, ukumbi wa magharibi hadi mashariki, Kenya nzima, kuna watu waliolazwa huko sasa yamkini 361 wakipata matibabu. Wengine wamekatwa miguu, mikono, wengine wamefanyiwa operesheni za tumbo na vichwa. Hivi sasa wako na majanga ya maumivu wakiwa wamelala katika hizo hospitali. Ni jambo la kusikitisha sisi kama Bunge tukiwa hapa kuona nchi yetu inaenda njia isiyo. Kuna umuhimu wa kurejesha nchi ili iende kwa njia inayofaaa. Kwanza, nchini Kenya, tuna vijana wadogo na barubaru wanaojulikana kama Gen. Z. Hawa vijana wamekuja kwenye maandamano barabarani wakiwa na chupa za maji kwa mkono wao wa kushoto na kwa mkono wa kulia, wameshika simu ili kurekodi historia wanapofanya maandamano wakidai haki za kila Mkenya zitendeke. Hawa vijana wa Gen Z hawana ukabila, ujamaa ama undugu. Wao wanajuana kama Wakenya. Wanajuana kama Wakenya walio ndugu mmoja, na wanaoishi pamoja katika nchi yao iliyojulikana kama Kenya. Hata Kenya ikiharibika, hawana nchi nyingine watakayoikimbilia. Kwa hivyo, wamekuja kutengeneza na kurekodi historia kwa sababu wanadai haki zao. Jambo la kusikitisha ni kuona polisi ambao ni utumishi kwa wote wakiongozwa na Inspekta Mkuu wa Polisi Bw. Koome wakitumia nguvu kupita kiasi kusimamisha maandamano haya yaliyo sababisha vifo na watu kuumia. Hivi sasa tunapoongea, kuna watu pengine wamekatwa miguu, mikono na hawajulikani watakavyopona. Ni jambo la kusikitisha. Nasema pole sana kwa wazee na akina mama wote. Sisi kama Seneti, tuko nanyi katika barabara hii. Tunaendelea kuunga mkono hao vijana kwa sababu maandamano yao yako katika Katiba na sheria. Inajulikana wazi ya kwamba, sababu ya kuwa na haya maandamano ni ule Mswada wa Fedha. Mswada huu ulikuwa na hesabu iliyokuwa sio sawa ya kutoza wananchi ushuru uliyopita kiasi. Tunajua ni jukumu la kila mwananchi kulipa ushuru, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}