GET /api/v0.1/hansard/entries/1442870/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442870,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442870/?format=api",
"text_counter": 66,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "lakini utozaji wa ushuru ukipita kiwango fulani, ama mambo yasiyofaa kutozwa ushuru yakiwekwa hapo, lazima watu waandamane ili kupata haki yao. Tunaona kabisa kwamba huu Mswada wa Fedha ulileta mushkin mkubwa nchini Kenya. Sisi hatuwezi kuwalaumu vijana wa Gen. Z kwa sababu walipokuja walisema Mswada huu unakandamiza kila mwananchi. Haukandamizi tajiri pekee, bali kila mtu nchini. Bw. Spika, sisi kama viongozi tunasema ya kwamba ni lazima tuwe na nidhamu. Hii ni kwa sababu tunaona wananchi wanaendelea kuishi maisha yasiyo mema. Maisha yamekuwa ghali na kila kitu katika nchi ya Kenya akipatikani Kumezuka majivuno na watu wanaojivunia sana ni wale ambao wanafanya ufisadi. Tumeona katika harakati za Wakenya ambao juzi na jana tulikuwa pamoja. Hivi leo, hawajamaliza miaka miwili ndani ya hili Bunge, lakini tunaona ya kwamba maisha yao yamegeuka. Wamekuwa matajiri zaidi ya vile inavyotakikana. Utajiri huu wanaupata kighafla ni kama mtu amechukua ndege na kupaa juu na kuwa tajiri mara moja kwa dakika 45, kisha kushuka chini kama mtu aliyefika Mombasa, ni hali ya aibu. Mambo kama haya ambayo tunaonyeshana ni ya kusikitisha. Kenya yetu inastahili amani. Tuliona hata balozi wa Uingereza akisema kwamba watu wamekuja hivi karibuni na walikuwa hawana chochote, lakini sasa wamekuwa matajiri mpaka wanatutapikia. Hii ndio maana Gen. Z wanasema aibu kama hii isitendeke katika nchi yetu. Bw. Spika, sisi tunasema ya kwamba vile ambavyo Mhe. Rais aliweza kukataa kupiga sahihi Mswada na akauregesha, ulikuwa mwelekeo wa kisawasawa. Serikali iweze kuangalia wale wamepoteza maisha yao pamoja na wale wote ambao wamepatwa na hasara katika maandamano haya. Sisi kama Bunge la Seneti tuko tayari wakati wowote. Hawa Gen Z. wakiwa wanataka kutuona sisi kama Bunge la Seneti tuko tayari. Waseme ni wapi na tuko tayari kuketi nao. Hakuna wakati Bunge hili la Seneti limehairishwa kwa sababu hatutaki kuonana na wananchi. Hata wakati wa vita, Bunge nyingi ulimwenguni huwa zimebaki zikisikiza wananchi. Hii ni kwa sababu Bunge ndio inaweza kutekeleza mwelekeo wa taifa. Hivi sasa, sisi tuko tayari. Tunasema poleni sana kwa wale ambao walipatwa na hasara ya maandamano. Kwa wale vijana wote wa Gen Z, Bunge la Seneti liko wazi na wakati wowote wakitaka kuonana na sisi, tuko tayari kukutana nao. Nimetangulia kusema ya kwamba kuna watu 39 ambao hivi sasa wamelala katika vyumba vya kuihifadhi maiti au mortuary . Hii ni kulingana na ratiba ya hesabu. Pia kunaweza kuwa kuna wengine zaidi katika pande mbalimbali za Kenya. Pia kuna wale ambao wameumia. Ni lazima hatua ichukuliwe dhidi ya polisi ambao walitumia bunduki za risasi badala ya kutumia bunduki ambayo inatupa mkebe wa kutoa machozi na kuwapiga hawa wananchi ambao walifariki. Washikwe na waweze kupelekwa kortini. Washtakiwe na makosa ya kutumia bunduki ama kutumia nguvu zaidi kuwaumiza wananchi ama kupoteza maisha yao. Wale wote ambao wameshikwa kiholela na wako korokoroni hivi sasa, kwa kutolewa katika gari kama vile tuliona yule Mbunge wa zamani alivyotolewa kutoka kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}