GET /api/v0.1/hansard/entries/1442873/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442873,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442873/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mhe. Rais amewaajiri watu ambao wako na rekodi za ufisadi katika Serikali yake. Kuna watu wamefanya vitendo vya uhalifu ambavyo havifai kulingana na sheria za Kenya. Mhe. Rais, ikiwa hao watu wako katika Serikali yako, afadhali uwaachishe kazi mara moja. Jambo lingine ni kwamba Mswada wa Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), hivi sasa uko kwenye mikono ya Mhe. Rais. Ni vizuri aupige sahihi ili kuondoa vuguvugu la kwamba hataki ama hawezi kupiga sahihi au kuna tashwishi yoyote. Hivi sasa, wananchi wanataka huo Mswada wa IEBC uwekwe sahihi na uwe sheria mara moja, ili mambo ya Kenya yaweze kuendelea na uchaguzi katika maeneo ambayo hayana wabunge au watu wanaowaakilisha. Kwa hivyo, aiweke kidole mara moja. Kuna wale walimu wa Junior Secondary School (JSS) na madaktari ambao wanamemaliza masomo na kupita mitihani yao. Hawa ni lazima waajiriwe mara moja. Pia ile programme ambayo ilikuwa inasaidia watoto wa watu wasiojiweza, kama vile,"
}