GET /api/v0.1/hansard/entries/1442877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1442877,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1442877/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, utakubaliana na mimi ya kwamba umeshakula chumvi ya kutosha. Mshahara hivi sasa ukae kando na wapee wale ambao hawajiwezi ili waweze kuendelea na maisha yao kisawasawa. Ama ile pesa ya mishahara, ipelekwa kwa hao ambao walipata majeruhi, wale ambao wamefariki na walio na shida. Ziende uko ili tuweze kuwasaidia. Bw. Spika, hii Hoja iko na maana sana. Sisi tunajua tuna uwiano. Tunajua sote ni Wakenya na Kenya ikiharibika, itakuwa ni nchi yetu imeharibika. Hatuna nchi nyingine ya kuenda isipokuwa kubaki hapa ndani ya nchi ya Kenya. Kwa hivyo, tunatakiana kila la heri kuona ya kwamba Serikali yetu na watu wetu wa Kenya tumekaa pamoja kama ndugu moja. Tuwe na amani na tupendane ili tuweze kurejesha nchi katika njia ya amani na mwelekeo. Asante. Naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}