GET /api/v0.1/hansard/entries/1443065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1443065,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443065/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Naunga mkono mazungumzo yanayoendelea hapa katika Bunge kuu la Seneti. Nashukuru sana Kiongozi wa Walio Wengi, Sen. Cheruiyot, kwa kuleta Hoja hii jana ili tuweze kuzungumza kuhusu nchi yetu. Tukiwa hapa, sisi ni Maseneta 67 na wamewakilisha kaunti 47. Sen. Cheruiyot, naomba kuwa miaka inayokuja utakuwa unaonekana katika nafasi za juu za uongozi wa nchi hii. Pili, ninatoa rambirambi zangu kwa familia ya wale vijana walioaga dunia. Walikufa wakati wa maandamano ya Gen Z. Kulikuwa na kilio kikubwa sana kwa sababu wengi walikuwa hawana familia, wazazi au mtu yoyote ambaye angeweza kuwasaidia. Vijana hawa wametoka kaunti mbalimbali. Kama Seneta wa kaunti ya Embu, natoa rambirambi zangu. Tatu, ningependa kusema kwamba kaunti zote zilizokuwa zimefanya maandamano ya amani lakini baadaye vijana wengi wakapata majeraha, mikono na miguu ilivunjika. Walipata shida nyingi sana kwa sababu ilikuwa kisa cha vuta nikuvute. Maandamano ya amani yaligeuka na kuwa mambo ya wizi kwa sababu ya wale waliojiunga na kikundi hicho. Maandamano haya yaligeuka kuwa kati ya askari na vijana. Pia walikuwa wanataka kupora mali. Mambo haya yalikumba kaunti za Mombasa, Migori, Kisumu, Nakuru, Nairobi na pia kaunti yangu. Kutoka siku hiyo, sikuweza kuenda Kaunti ya Embu. Ningependa kuwaambia watu wa Embu Kaunti pole kwa sababu ya yale yaliyotendeka. Hatujawahi kuona mambo kama hayo. Zile pesa za devolution tumekuwa tunapokea kwa miaka 10 zimekuwa na shida kwa sababu zililiwa na wale matapeli ambao walikuwa wanaongoza. Katika hii Serikali ya Kenya Kwanza, mimi nilichaguliwa na wananchi ili nije kuwawakilisha. Nilileta amani ndio sababu wanasema kuwa watu wawili hawawezi kukosa kuelewana. Sisi kama Maseneta, magavana na wale viongozi wengine tulisema tutatembea barabara moja. Jambo la ajabu ni kwamba wakati tulikuwa tunaendelea kufufua uchumi wa Embu, wale watu waliokuwa na nia mbaya walitoka kwenye kona zingine nje ya kaunti na wakachoma ofisi ya Gavana ambayo ilikuwa renovated na zile pesa. Haya ni mambo ya ajabu. Wale watu hawakuwa na adabu wala heshima kwa Kaunti ya Embu kwa sababu hata magari ya wafanyikazi wa Serikali ya Kaunti ya Embu pia yalichomwa. Tulishindwa kwa sababu hao watu hawakuwa wakati wa kupitisha bajeti na wala hawakuikubali wala kuikataa. Hatukuona Gavana wetu akienda kusema ‘yes’ or ‘no.’ Hii ilikuwa ni shida. Nawaambia pole sana na tutarekebisha mambo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}