GET /api/v0.1/hansard/entries/1443066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1443066,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1443066/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo la ajabu ni kuwa zile pesa tulizotarajia zije tarehe moja, hazitatumika kufanya kazi katika kaunti; sasa zitaenda kurekebisha ofisi ya Gavana ambayo ilichomwa. Sisi kama watu wa Kaunti ya Embu, tumerudi nyuma sana. Wale matapeli waliokuwa wamepanga hayo mambo walifanya makosa. Walienda pia kwa KRA na kuwasha moto. Walifanya makosa kuchoma majengo ambayo maafisa wa KRA wanafanyia kazi. Huo ni ushuru wetu ambao utatumiwa kujenga mpya hayo. Kuna kitendo walichofanya katika Kaunti ya Embu. Hayo ni mambo ya ajabu sana. Kuna Kenyatta School ambayo ni shule ya watoto walemavu. Walienda kule na kuwasha moto usiku wa manane. Nilishindwa kujua kama yalikuwa maandamano au wizi. Nawapa pole watu wa sub county hiyo katika Kaunti ya Embu. Katika Isaya 1:18, maandiko yanasema kuwa watu wawili hawawezi kutembea pamoja bila kuelewana. Kuna pahali pia wanasema: Njoo tusemezane. Ningependa kuwaambia Maseneta, Wabunge, Gen Z, makanisa na watu wote kwa jumla, kuwa tunafaa kuombea nchi yetu ya Kenya kwa sababu ya mambo ambayo yamefanyika. Naomba viongozi wote. Unaweza kuwa uliteuliwa na Mhe. Rais ama ulipewa kazi na mtu mwingine. Unafaa kujua kuwa una bahati kwa sababu kuna watu wengine wengi ambao wanaweza kufanya kazi hiyo. Kwa hivyo, unafaa kumshukuru Mungu. Nataka kuwaambia Gen Z na watu wengine kwamba tumesikia kilio chao. Ni muhimu kuelewana ili tuweze kukuza uchumi wa Kaunti ya Embu. Ninataka kuzungumza kuhusu vijana wetu ambao walikuwa wanagoma. Baadhi yao wako katika vyuo vikuu na wengine katika shule za sekondari. Tunajua kwamba wana elimu ya kutosha ya kuwawezesha kufanya kazi yoyote katika nchi yetu ya Kenya. Ninaomba mguzwe na Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Tunaamini Mungu mmoja. Msikubali tena kufanya maandamano. Tumesikia Mhe. Rais wetu akizungumza. Alisema anataka kufanya mazungumzo na watu wote ikiwemo vijana. Kuna mambo yaliyokuwa kule Nyahururu. Hata nyuki akitoka nje, lazima atarudi kwenye mzinga. Naunga mkono kwamba Mhe. Rais William Samoei Ruto na Naibu wake, Mhe. Rigathi Gachagua, wanafaa kuketi chini na kuzungumza. Pia, wanafaa kuongea na viongozi wote ili tuone jinsi ya kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Kuna mambo mengi ambayo yamesemwa. Tumeongea kuhusu mambo ya kuketi pamoja na kutafuta nafasi za kazi. Kabla sijayazungumzia, ningependa kuongea kuhusu mambo ya kazi. Sisi kama Maseneta lazima tufanye kazi inayofaa. Wakati mwingine tunapigana hapa kwa midomo. Ningependa kuwaambia Wakenya kwamba tuko Maseneta 67 na tunaongea lugha moja. Hakuna mambo ya Azimio la Umoja-One Kenya Coalition wala Kenya Kwanza Alliance. Sisi sote tunasema Mungu mbele. Kuna mambo lazima tuyafikirie kama Maseneta. Tusipochunga, tunaweza kuanza kupigana. Kuna ajenda mbili muhimu za Gen Z. Wengine wakiulizwa kwa nini wanafanya hivyo, wanasema kuwa hawataki kuoa wala kuolewa kwa sababu wanapitia shida nyingi. Wengine wanasema kuwa wamesoma na wana digrii tano au hata 10 na wamekaa miaka mingi bila kupata kazi. Kwa hivyo, wamepoteza matumaini. Nataka kuwaambia Wakenya kwamba vijana wetu wengi ndio wameaga dunia. Hilo ni jambo la kuhuzunisha. Katika Biblia, kuna wakati watoto wote wa kwanza wa kiume walikuwa wanauawa kule Misri. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}